KILAKALA AIPONGEZA WIZARA YA NISHATI KUENDELEA KUTOA ELIMU YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

KILAKALA AIPONGEZA WIZARA YA NISHATI KUENDELEA KUTOA ELIMU YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Mussa Kilakala, ameipongeza Wizara ya Nishati kwa kuandaa Warsha ya Nishati Safi ya Kupikia kwa wanahabari na Maafisa habari, akisema mafunzo hayo ni hatua muhimu ya kuhakikisha elimu sahihi inawafikia wananchi na kuimarisha utekelezaji wa ajenda ya matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini. Akizungumza Julai 14, 2026 wakati wa ufunguzi wa Warsha ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari, Maafisa Mawasiliano Serikalini wa Mikoa, Taasisi, Wizara pamoja na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati kuhusu uandishi na uhamasishaji wa masuala ya nishati safi ya kupikia inayofanyika katika Ukumbi wa Morena Hotel mkoani Morogoro amesema Mkoa wa Morogoro una vyanzo vingi vya maji vinavyopaswa kulindwa, hivyo ajenda ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia itasaidia kuhifadhi mazingira kwa kupunguza ukataji wa miti, kulinda afya za wananchi pamoja na kutunza vyanzo hivyo vya maji kwa manufaa ya kizazinkijacho. Amesema elimu inayotolewa kupitia warsha hi…