KIGOMA: LANGO JIPYA LA BIASHARA UKANDA WA MAZIWA MAKUU NA KUSINI MWA AFRIKA
KIGOMA: LANGO JIPYA LA BIASHARA UKANDA WA MAZIWA MAKUU NA KUSINI MWA AFRIKA Kwa miaka mingi, kulikuwa na msemo uliokuwa ukivuma kwamba “Kigoma ni mwisho wa reli.” Ingawa ulitamkwa kwa utani, kwa kiasi kikubwa uliakisi hali halisi ya miundombinu na mtazamo uliokuwepo kuhusu mkoa huo. Wengi waliiona Kigoma kama eneo la mwisho wa safari badala ya lango la biashara na uchumi. Licha ya kuwa na Bandari ya Kigoma katika Ziwa Tanganyika na kupakana na masoko makubwa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Burundi na Zambia, uwezo wake wa kuchochea biashara ya kikanda ulikuwa mdogo kutokana na changamoto za miundombinu ya usafirishaji. Gharama kubwa za kusafirisha mizigo, safari ndefu na kutokuwepo kwa mfumo wa kisasa wa uchukuzi vilifanya fursa nyingi za kiuchumi zibaki bila kutumika ipasavyo. Hata hivyo, taswira hiyo inaanza kubadilika kupitia mkakati wa Serikali ya Awamu ya Sita wa kuwekeza kwa wakati mmoja katika Reli ya Kisasa (SGR), bandari, usafiri wa majini, viwanja vya ndege na huduma nyingine za msingi. Badala ya kutekeleza miradi kama miradi ya kawaida ya…