KATIBU MWENEZI MKOA WA IRINGA  AHIMIZA UMOJA WA KIDINI, ACHANGISHA MILIONI 19

KATIBU MWENEZI MKOA WA IRINGA  AHIMIZA UMOJA WA KIDINI, ACHANGISHA MILIONI 19
NA DENIS MLOWE, IRINGA KATIBU wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Mkoa wa Iringa, Joseph Ryata, amewapongeza viongozi mbalimbali wa kitaifa kwa mchango wao katika ujenzi wa Kanisa la Lutheran Mlandege akisema ushirikiano wao unaonyesha namna Watanzania wanavyoweza kushirikiana bila kujali tofauti za dini. Ryata alitoa kauli hiyo alipokuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Mjumbe Kamati ya Siasa Mkoa wa Iringa Dickson Mwipopo katika ibada kuchangisha yenye lengo la ikununua basi aina ya Costa kwa ajili ya kwaya ya usharika ya kanisa la Lutherani Mlandege na kufanyika Kanisani hapo ambapo alisema viongozi hao walitoa mchango mkubwa kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa nyumba ya ibada kwa kutambua umuhimu wa kumtumikia Mungu na kuimarisha mshikamano wa kitaifa. Katika zoezi hilo la uchangiaji Jumla sh. million 19,5,40,000 zilipatikana ikiwa ni ahadi pamoja na fedha taslimu ambapo wadau mbalimbali walijitokeza kuchangia kanisa hilo ambapo  mjumbe wa kamati ya siasa ya Ccm Mkoa wa Iringa Dickson Mwipopo…