KATIBU MKUU WA OACPS AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI

KATIBU MKUU WA OACPS AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Afrika, Karibiani na Pasifiki (OACPS), Mhe. Moussa Saleh Batraki, amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku nane kuanzia Julai 19 hadi 26, 2026, ikiwa ni ziara yake ya kwanza nchini tangu alipoanza kutekeleza majukumu hayo mwezi Machi 2025. Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Mhe. Batraki alipokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji na Mkuu wa Ujumbe wa Tanzania katika Umoja wa Ulaya, Mhe. Jestus Nyamanga, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Ellen Maduhu, pamoja na maafisa wengine kutoka Wizara hiyo. Akiwa nchini, Katibu Mkuu huyo anatarajiwa kufanya mazungumzo ya ngazi ya juu na viongozi wa Serikali jijini Dar es Salaam na Zanzibar, ikiwa ni pamoja na kukutana na Wabunge na Mawaziri wenye dhamana ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mifugo na Uvuvi, pamoja na Uchumi wa Buluu. Aidha, Mhe. Batraki anatarajiwa kutem…