KATIBU CCM KILOSA ATUHUMIWA KUTISHIA MAISHA MWANACHAMA
Na Mwandishi Wetu KATIBU wa Chama cha Mapinduzi (CCM)Wilaya ya Kilosa,Mkoani Morogoro, Janus Mfaume, anatuhumiwa kumdhalilisha na kumtishia maisha mwanachama wa Chama hicho Egon Haule, baada ya kumfukuza ofisini bila sababu za msingi huku akimtolea kauli za vitisho. Tukio hilo limetokea Julai 17 mwaka huu katika ofisi za Wilaya za Chama hicho ambapo Haule alikwenda kuitikia wito wa Katibu wa Jumuiya ya Wazazi aliyemwita kwa ajili ya kumpa majukumu. Akizungumza kwa masikitiko makubwa Haule,alisema,hii ni mara ya tatu anafanyiwa udhalilishaji na kutishiwa maisha na Mfaume huku akitishia kumfanyia kitu kibaya ambacho hata kisahau katika maisha yake. Haule alisema,hana ugomvi wowote na Katibu wake huyo lakini anashangazwa kuona kila siku amekua akimtishia maisha sambamba na kumfukuza kufika katika ofisi za Chama hicho Wilaya. “Mimi ni mwanachama halali ambaye nimekua nikijitolea majukumu mbalimbali ya Chama kwa mwamvuli wa UVCCM Wilaya lakini napitia manyanyaso na udhalilishaji kwa kufukuzwa k…