Katambi-Hatutacheka na mtu Anaehatarisha Usalama wa Raia
Katambi-Hatutacheka na mtu Anaehatarisha Usalama wa Raia
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Patrobas Katambi baada ya tafiti, kubadilishana uzoefu na stadi mbalimbali kutoka kwa Nchi zenye mbinu bora,teknolojia ya juu pamoja na uzoefu mkubwa wa kukabiliana na uhalifu,Amezindua Programu Maalumu ya Usalama,Maendeleo na Samia ambayo pia itashirikisha hatua za Mafunzo na Vifaa vya Kisasa kutoka nchi zilizoendelea Kiusalama lengo ikiwa ni kuimarisha na kuhusianisha Usalama na masuala ya Amani na Maendeleo Tanzania bara na visiwani . Waziri Katambi amezindua Programu hiyo leo,jijini Dar es Salam katika Viwanja vya Mnazi Mmoja ambapo akizungumza na mamia ya wafanyabiashara,machinga,madereva bodaboda,mamalishe na babalishe amesema suala la amani na usalama ni jukumu la kikatiba la serikali iliyochaguliwa na wananchi. Amesisitiza kuwa kipaumbele cha Rais Samia ni Nchi Kwanza, Wananchi kwanza na Uchumi kwanza. “Wizara hii ina dhamana ya masuala ya Ulinzi na Usalama, ina dhamana ya ulinzi wa kila raia, ina dhamana ya ulinzi wa kila mali ya raia, ina dham…