KAPINGA: WATANZANIA WAJITOKEZE SABASABA, BIDHAA ZA NDANI ZAZIDI KUBOREKA
KAPINGA: WATANZANIA WAJITOKEZE SABASABA, BIDHAA ZA NDANI ZAZIDI KUBOREKA Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga (Mb), amewataka Watanzania kuendelea kutembelea Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), akisema maonesho ya mwaka huu 2026 yameonesha mafanikio makubwa ya maendeleo ya viwanda, ubunifu wa teknolojia na ubora wa bidhaa zinazozalishwa nchini. Akizungumza Julai 08, 2026 baada ya kutembelea mabanda mbalimbali ya maonesho hayo, Kapinga amesema mwitikio wa wananchi ni mkubwa kiasi kwamba Serikali inatafakari kuongeza siku moja ya maonesho ili kutoa nafasi kwa wananchi wengi zaidi kushiriki na wafanyabiashara kuendelea kufanya biashara. Amesema ukubwa wa maonesho hayo unamlazimu kuyatembelea mara kwa mara kwa kuwa haiwezekani kuona mabanda yote kwa siku moja, huku akieleza kuridhishwa na namna waoneshaji walivyojiandaa na ubora wa bidhaa zinazooneshwa. Waziri Kapinga amesema maonesho ya mwaka 2026 yamebeba teknolojia mbalimbali za kisasa, ikiwemo magari yanayotumia umeme, magari ya mseto (hybrid), magari yanayotumia…