JESHI LA POLISI MBEYA LAWASHUKURU WADAU NA WANANCHI KWA USHIRIKIANO.
JESHI LA POLISI MBEYA LAWASHUKURU WADAU NA WANANCHI KWA USHIRIKIANO.
Katika kuhakikisha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linatoa huduma bora kwa wananchi kwa kutumia vifaa vya kielektroniki pamoja na mifumo mbalimbali ya kidigitali, wananchi na wadau Mkoani humo wapongezwa kwa kuendelea kushirikiana na Jeshi hilo katika kuzuia na kutokomeza uhalifu. Hayo yamesemwa na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Wilbert Siwa Julai 21, 2026 wakati akipokea msaada wa "Computer" iliyotolewa na Diwani wa Kata ya Ilemi kwa ajili ya kusaidia kazi za Polisi Jamii Wilaya ya Mbeya. "Msaada huu umekuja wakati muafaka ambapo Jeshi la Polisi nchini limejikita katika matumizi ya mifumo mbalimbali ya kidigitali katika utendaji wake wa kazi, hivyo vifaa hivi vitasaidia kuongeza ufanisi na weledi katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali" alisema Kaimu Kamanda Siwa. Aidha, Kaimu Kamanda Siwa amesema kuwa elimu inayotolewa na Polisi na Wakaguzi Kata kwa makundi mbalimbali imesaidia wananchi kujua wajibu wao na kuzaa matunda ikiwe…