JAB YAPOKEA OMBI LA KUTOA MAFUNZO KWA BLOGGERS ZAIDI YA 200
JAB YAPOKEA OMBI LA KUTOA MAFUNZO KWA BLOGGERS ZAIDI YA 200 Na Mwandishi Wetu, JAB Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imepokea ombi kutoka Mtandao wa Mabloga Tanzania (TBN) la kutoa mafunzo kwa wanachama wake zaidi ya 200 kuhusu Sheria ya Huduma za Habari, Maadili ya Uandishi wa Habari na umuhimu wa kupata ithibati. Ombi hilo limetolewa leo, tarehe 16 Julai, 2026, na Mwenyekiti wa Mtandao wa Mabloga Tanzania, Bw. Beda Msimbe, alipokutana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa JAB, Wakili Patrick Kipangula, katika mazungumzo yaliyofanyika katika ofisi za Bodi jijini Dar es Salaam. Akizungumza baada ya mazungumzo hayo, Wakili Kipangula amesema Bodi imepokea ombi hilo na iko tayari kushirikiana na Mtandao huo katika kuwawezesha bloga kupata uelewa wa kina kuhusu Sheria ya Huduma za Habari, maadili ya taaluma pamoja na umuhimu wa kupata ithibati. Amesema mafunzo hayo yataanza kutolewa kwa bloggers wenye ithibati ili kuimarisha weledi na uelewa wao wa majukumu ya kitaaluma, kabla ya kuendelea kuwafikia wale ambao bado hawajapata ithibati. “Wale ambao ha…