HUKUMU YA TIKTOKER GHANA: SOMO KWA UHURU WA KUJIELEZA NA WAJIBU WA WATUMIAJI WA MITANDAO
HUKUMU YA TIKTOKER GHANA: SOMO KWA UHURU WA KUJIELEZA NA WAJIBU WA WATUMIAJI WA MITANDAO
Hivi karibuni, Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Accra ilimuhukumu Camilla Alhassan, mshawishi maarufu wa TikTok (Tiktoker), kifungo cha mwaka mmoja jerezani. Adhabu hii ilitolewa baada ya mshtakiwa kukiri makosa ya kusambaza taarifa za uongo na kufanya tabia ya kuudhi (offensive conduct) dhidi ya Rais John Dramani Mahama. Kesi hii inaashiria hatua kubwa katika udhibiti wa maudhui ya kidijitali barani Afrika na inaibua maswali muhimu kuhusu mipaka ya uhuru wa kujieleza na wajibu wa kisheria wa watumiaji wa mitandao ya kijamii. Hukumu dhidi ya Alhassan inasimama juu ya misingi miwili mikuu ya kisheria inayolenga kulinda usalama wa jamii na sifa za watu Mosi, Kusambaza Taarifa za Uongo (False News) - Sheria za Ghana zinakataza utengenezaji au usambazaji wa taarifa ambazo mtengenezaji anajua au ana sababu ya kuamini kuwa ni za uongo, hususan kama zinaweza kusababisha hofu au taharuki miongoni mwa jamii. Pili, Tabia ya Kuudhi (Offensive Conduct) - Matumizi ya lugha au madai yanayolenga kudhalili…