HARAKATI ZINAZOONGOZWA KUTOKA UGHAIBUNI ZAKOSA MWITIKIO NDANI YA TANZANIA
HARAKATI ZINAZOONGOZWA KUTOKA UGHAIBUNI ZAKOSA MWITIKIO NDANI YA TANZANIA
Maandamano ya Julai 7 yaliyohamasishwa kupitia mitandao ya kijamii yalitarajiwa kuwa na mwitikio mkubwa kutoka kwa wananchi. Hata hivyo, siku hiyo haikuwa kama ilivyotarajiwa na waandaaji wake. Badala ya wananchi kujitokeza kwa wingi, wengi walibaki majumbani huku wengine wakifunga biashara zao kutokana na hofu ya usalama na sintofahamu iliyokuwepo. Wachambuzi wa masuala ya kijamii wanaeleza kuwa moja ya sababu zilizochangia hali hiyo ni ukweli kwamba viongozi wengi wa harakati hizo wanaishi nje ya Tanzania. WANAHARAKATI WENGI WANAISHI UGHAIBUNI Kwa miaka kadhaa sasa, wanaharakati wengi wa Kitanzania wamekuwa wakiishi nje ya nchi. Wapo walioondoka kutokana na changamoto za kisiasa, masuala ya usalama pamoja na kutafuta maisha bora. Mfano unaotolewa mara nyingi ni wa Tundu Lissu aliyelazimika kuondoka nchini baada ya kushambuliwa kwa risasi wakati wa utawala wa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli. Baada ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuingia madarakani, Lissu alirejea nchini na kuendelea na sh…