HALMASHAURI MERU YADAIWA KUVAMIA ARDHI YA WANANCHI, RAIS AOMBWA KUINGILIA KATI

HALMASHAURI MERU YADAIWA KUVAMIA ARDHI YA WANANCHI, RAIS AOMBWA KUINGILIA KATI
Na Mwandishi wetu. Arusha. Wamiliki wa Ardhi na Makazi  eneo la Kitongoji cha Relini na Mariton ,kijiji cha Malula Kata ya Malula Wilaya ya Arumeru ,mkoa Arusha, wameomba Rais Samia Suluhu Hassan, kuingilia kati kuzuia Uvamizi wa ardhi yao zaidi ya hekali 3000 unaofanywa na  Halmashauri ya Meru. Wananchi hao ,wamesema baadhi yao  licha ya kushinda kesi mahakama ya rufaa na wengine kesi zikiwa bado zipo mahakamani,wameshangazwa na uamuzi wa halmashauri kuvamia eneo hilo kuanza kupima na kuweka bicon wakitumia polisi kuimarisha ulinzi katika ardhi yao.                Halmashauri Yakiri kuvamia ardhi na licha uwepo wa kesi. Hata hivyo, Mwanasheria wa halmashauri hiyo,Jonathan Kiama akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa halmashauri ya Meru, kuhusiana na mgogoro huo, licha ya kukiri uwepo wa kesi Mahakama na kesi nyingine kumalizika katika mahakama ya rufaa kwa familia ya Okash kukabidhiwa ardhi, alisema ardhi hiyo ni mali ya halmashauri na sio ya wananchi. "Sisi tunapima na kuweka alama …