ETDCO, SONELGAZ YA ALGERIA ZAIBUA FURSA ZA USHIRIKIANO KATIKA USAFIRISHAJI UMEME

ETDCO, SONELGAZ YA ALGERIA ZAIBUA FURSA ZA USHIRIKIANO KATIKA USAFIRISHAJI UMEME
Balozi Mobhare Matinyi (wa tano kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya ETDCO, ambayo ni kampuni tanzu ya TANESCO waliokuwa ziarani nchini Algeria. Kulia kwa Balozi Matinyi ni Mwenyekiti wa bodi hiyo, Bw. Raymond Mbilinyi.  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Usafirishaji na Usambazaji wa Umeme nchini (ETDCO), Bw. Raymond Mbilinyi, ameahidi kushirikiana na Shirika la Umeme na Gesi la Algeria (SONELGAZ) katika teknolojia ya kisasa ya usafirishaji na usambazaji wa umeme ili kuboresha huduma hiyo nchini. Akizungumza na Balozi Mobhare Matinyi katika ofisi za Ubalozi wa Tanzania jijini Algiers tarehe 25 Julai, 2026, Bw. Mbilinyi alisema ziara yao ya wiki moja imewapatia mwanga kuhusu teknolojia ya kisasa ya usafirishaji na usambazaji wa umeme inayozingatia ubora wa huduma na utunzaji wa nishati. Bw. Raymond alimfahamisha Balozi Matinyi kwamba kupitia ziara hii waliona fursa nyingi za ushirikiano na Sonelgaz kupitia kampuni yake ya Sonelgaz I…