DKT. NCHIMBI: WATANZANIA PAMBANENI KUPATA KATIBA MPYA YENYE MWAFAKA ITAKAYODUMU MIAKA 50
DKT. NCHIMBI: WATANZANIA PAMBANENI KUPATA KATIBA MPYA YENYE MWAFAKA ITAKAYODUMU MIAKA 50
Na Janeth Raphael - MichuziTv Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amesema ikiwa angepewa nafasi ya kutoa ujumbe mmoja wa mwisho kwa Watanzania, basi usingekuwa mwingine zaidi ya kuwahimiza kuendelea kupambana kwa ajili ya kupata Katiba Mpya itakayokuwa na mwafaka wa kitaifa na kudumu kwa angalau miaka 50 ijayo. Dkt. Nchimbi ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu, ambapo alizungumzia historia ya safari ya Tanzania kuelekea kupata Katiba Mpya na umuhimu wa kuendelea kujenga maridhiano katika mchakato huo. Amesema mjadala kuhusu Katiba Mpya si wa leo wala wa jana, bali ni ajenda ambayo imeendelea kujadiliwa kwa zaidi ya miongo minne, huku akieleza kuwa vuguvugu la kuisukuma kwa nguvu lilianza mwaka 1992 baada ya kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa. Kwa mujibu wa Makamu wa Rais, Tanzania imepitia hatua mbalimbali katika kutafuta Katiba …