DKT. MWIGULU: FEDHA ZA MARATHON ZILETE TIJA KWA WALENGWA
DKT. MWIGULU: FEDHA ZA MARATHON ZILETE TIJA KWA WALENGWA *Serikali kuendelea kuboresha miundombinu wezeshi Mkoani Dodoma. Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba amezitaka wizara na taasisi zinazonufaika na fedha za NBC Marathon zihakikishe zinatumika kwa uwazi na kwa kuzingatia thamani ya fedha, ili malengo yaliyokusudiwa yaweze kuleta matokeo, tena matokeo yanayopimika. Amesisitiza kuwa kila shilingi inayowekezwa katika mbio hizo zinapaswa kuleta matokeo yanayoonekana, kwa sababu unaposhughulika na masuala ya afya, unaongelea uhai wa Watanzania. Aidha Waziri Mkuu amesema kuwa NBC Dodoma Marathon imeendelea kuwa zaidi ya mashindano ya riadha kwa kuwa ni jukwaa muhimu la kuhamasisha afya, kuimarisha ustawi wa jamii na kuchangia mapambano dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi pamoja na kuboresha huduma za afya nchini. Dkt. Nchemba amesema hayo leo Julai 26, 2026, alipokuwa Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa msimu wa saba wa NBC Dodoma Marathon uliofanyika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, ukiwa na kaulimbiu ya #KataWeseOkoaMaisha. Akizungumza katika hafla h…