DKT. MWIGULU AALIKA WAFANYABIASHARA WA UFARANSA KUWEKEZA TANZANIA

DKT. MWIGULU AALIKA WAFANYABIASHARA WA UFARANSA KUWEKEZA TANZANIA
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, amewaalika wafanyabiashara wa Ufaransa kuwekeza Tanzania, akisisitiza kuwa mazingira mazuri ya uwekezaji yaliyopo nchini yanatoa fursa kubwa za kukuza biashara, kuzalisha ajira, kuhamisha teknolojia na ujuzi, pamoja na kuharakisha ujenzi wa uchumi wa viwanda wenye manufaa kwa Tanzania na Ufaransa. Akizungumza Julai 6, 2026, katika Mjadala wa Kibiashara kati ya Tanzania na Ufaransa (Tanzania–France Business Roundtable) uliofanyika katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania jijini Paris, Dkt. Mwigulu alisema ushirikiano wa kiuchumi kati ya sekta binafsi za nchi hizo mbili unafungua ukurasa mpya wa uwekezaji na biashara. “Leo tumefanya mjadala wa kibiashara na sote tumeshuhudia makubaliano yakisainiwa kati ya Tanzania Private Sector Foundation (TPSF) na International Chamber of Commerce (ICC) ya Ufaransa. Makubaliano haya si mkataba wa kawaida, bali ni daraja litakalotupeleka kwenye mafanikio makubwa ya kiuchumi na kibiash…