DIRA YA MAENDELEO YA TAIFA 2050 YAIPA SEKTA YA MADINI MWELEKEO MPYA WA KUCHOCHEA UCHUMI
DIRA YA MAENDELEO YA TAIFA 2050 YAIPA SEKTA YA MADINI MWELEKEO MPYA WA KUCHOCHEA UCHUMI
📍Dar es Salaam Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Dkt. Janet Lekashingo, amesema Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 imeipa sekta ya madini nafasi ya kimkakati ya kuongoza mageuzi ya uchumi wa Tanzania kupitia uongezaji thamani wa madini, ushirikishwaji wa watanzania na matumizi ya teknolojia za kisasa katika shughuli za uchimbaji wa madini. Akizungumza mapema leo Julai 6, 2026, alipotembelea mabanda ya taasisi zilizo chini ya Wizara ya Madini katika Kijiji cha Madini kwenye Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), Dkt. Lekashingo amesema Tume ya Madini imejipanga kikamilifu kutekeleza malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 ili sekta ya madini iwe nguzo muhimu ya ukuaji wa uchumi na maendeleo endelevu. Amesema utekelezaji wa dira hiyo unalenga kuongeza thamani ya madini ndani ya nchi badala ya kuyasafirisha ghafi, kuimarisha utafiti wa jiolojia ili kubaini maeneo mapya yenye rasilimali za madini, kuongeza ushiriki wa watanzania katika miradi ya uchimbaji wa madin…