DCEA: JITIHADA ZA SERIKALI ZAPUNGUZA KWA KIASI KIKUBWA KILIMO CHA BANGI MARA

DCEA: JITIHADA ZA SERIKALI ZAPUNGUZA KWA KIASI KIKUBWA KILIMO CHA BANGI MARA
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo, amesema kilimo cha bangi katika Mkoa wa Mara kimepungua kwa takribani asilimia 80 kutokana na operesheni endelevu zinazotekelezwa na Serikali katika kukabiliana na uzalishaji wa dawa za kulevya. Akizungumza leo, Julai 24, 2026, baada ya kuhitimisha operesheni maalumu zilizofanyika katika Wilaya za Tarime na Rorya, Lyimo alisema operesheni hizo zimefanikisha kuteketezwa kwa mashamba ya bangi yenye ukubwa wa ekari 291.2, kukamatwa kwa magunia 15 ya bangi kavu pamoja na pikipiki nne zilizokuwa zikitumika katika shughuli hizo haramu. Aidha, watu wawili wamekamatwa huku uchunguzi ukiendelea kuwabaini na kuwakamata washirika wengine waliohusika katika mtandao huo. Alisema mafanikio hayo yanathibitisha ufanisi wa operesheni za Serikali, akibainisha kuwa mwaka 2024 zaidi ya ekari 3,500 za mashamba ya bangi ziliteketezwa katika Mkoa wa Mara. Hatua hiyo, alisema, imechangia kwa kiwango kikubwa kupunguz…