Posts

CHATILA AFUNGUKA MIPANGO YA KUIBADILI UJENZI SPORTS CLUB

CHATILA AFUNGUKA MIPANGO YA KUIBADILI UJENZI SPORTS CLUB
Na. Mtemi Sona Dodoma. Mwenyekiti wa Ujenzi Sports Club, Arch. Ibrahim Chatila, amesema uongozi mpya umejipanga kuijenga timu hiyo kuwa ya kisasa, imara na yenye ushindani mkubwa katika mashindano yote itakayoshiriki. Akizungumza kuhusu mikakati ya kuiboresha klabu hiyo iliyo chini ya Wizara ya Ujenzi, Chatila amesema lengo kuu ni kuunda kikosi chenye ubora wa hali ya juu kitakachokuwa na uwezo wa kushindana na timu mbalimbali nchini. Amesema hatua za awali zitahusisha usajili wa wachezaji bora pamoja na kuimarisha benchi la ufundi kwa kuwashirikisha makocha wenye uwezo na sifa zinazohitajika ili kuongeza ushindani wa timu. "Tunataka kuunda timu yenye wachezaji watakaoweza kuleta ushindi na ambao watazingatia weledi, nidhamu na taaluma katika kila mashindano tutakayoshiriki," amesema Chatila. Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa uongozi mpya uliochaguliwa umeazimia kuijenga upya Ujenzi Sports Club kwa misingi ya umoja, utawala bora na uwajibikaji kuanzia kwa viongozi, benchi la ufundi,…