CHATANDA: GAWIO LA TRILIONI 1.3 KIELELEZO CHA UIMARA WA SERIKALI KATIKA KUKUZA MAENDELEO
CHATANDA: GAWIO LA TRILIONI 1.3 KIELELEZO CHA UIMARA WA SERIKALI KATIKA KUKUZA MAENDELEO
NA MWANDISHI WETU, DODOMA Taasisi, mashirika ya umma na kampuni ambazo serikali ina hisa chache zimefanikiwa kuwasilisha gawio kwa serikali lenye thamani ya shilingi trilioni 1.3. Uwasilishaji huo umefanyika Juni 30, 2026, katika Ikulu ya Dar es Salaam, ambapo Rais Dk. Samia Suluhu Hassan alihudhuria hafla hiyo . Mbunge wa Viti Maalum wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mwenyekiti Taifa wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Mary Chatanda amesema, gawio la shilingi trilioni 1.3, ni udhihirisho wa uimara wa serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi wake. "Tumeshuhudia taasisi na mashirika ya umma yakitoa gawio la shilingi trilioni 1.3, hizi ni fedha nyingi sana hasa unapoziingiza katika mzunguko wa shughuli za kiuchumi na uboreshaji wa huduma za kijamii, lazima zilete tija katika maisha ya wananchi," amesema Chatanda. Sambamba na hilo, Chatanda amesema, mafanikio hayo hayawezi kutenganishwa na uongozi thabiti wa Rais Dk. Samia ambaye daima amekuwa akitoa maelekezo mazuri ya namna bo…