BIASHARA YA MAZAO YAPAA KUPITIA STAKABADHI ZA GHALA, WAKULIMA WAINGIZA SH. TRILIONI 2.3
BIASHARA YA MAZAO YAPAA KUPITIA STAKABADHI ZA GHALA, WAKULIMA WAINGIZA SH. TRILIONI 2.3
Na Dotto Kwilasa, Dodoma Biashara ya mazao kupitia Mfumo wa Stakabadhi za Ghala imeendelea kushika kasi nchini baada ya wakulima kuuza zaidi ya kilo bilioni 1.122 za mazao na kuingiza Shilingi trilioni 2.298 katika mwaka wa fedha 2025/26, ikiwa ni ongezeko la asilimia 43.6 ikilinganishwa na mwaka uliotangulia. Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB), Asangye Bangu, alisema Julai 31, 2026 jijini Dodoma kuwa ongezeko hilo linaakisi kuimarika kwa matumizi ya mfumo huo, ambao umeendelea kuwapa wakulima fursa ya kuuza mazao kwa ushindani na uwazi kupitia minada ya kidijitali. Alisema mazao tisa yaliuzwa kupitia mfumo huo, yakiwemo korosho, mbaazi, ufuta, kahawa, kakao, dengu, choroko, soya na chai, huku korosho zikiongoza kwa kiasi kilichouzwa, zikifuatiwa na mbaazi na ufuta. Bangu alisema mafanikio hayo yamewanufaisha pia Halmashauri zilizokusanya Shilingi bilioni 61.05 kupitia ushuru wa mazao (CESS), wakati thamani ya biashara yote iliyofanyika kupitia mfumo h…