AZZA AZINDUA VITUO VYA BODABODA TINDE : TUILINDE AMANI, HATUNA SEHEMU YA KUKIMBILIA ZAIDI YA MAMA TANZANIA
AZZA AZINDUA VITUO VYA BODABODA TINDE : TUILINDE AMANI, HATUNA SEHEMU YA KUKIMBILIA ZAIDI YA MAMA TANZANIA
Mbunge wa Jimbo la Itwangi, Mhe. Azza Hillal Hamad, akiwa pamoja na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga, Edward Ngelela (kulia), wakikagua moja ya vituo vya waendesha bodaboda vilivyozinduliwa katika Kata ya Tinde, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga. Vituo hivyo vimetengenezwa na Mhe. Azza Hillal Hamad kwa ajili ya kuwawezesha waendesha bodaboda kufanya shughuli zao katika mazingira rasmi na yenye utaratibu. Mbunge wa Jimbo la Itwangi, Mhe. Azza Hillal Hamad, akizungumza leo Julai 18, 2026 wakati wa uzinduzi wa vituo vitatu vya waendesha bodaboda alivyovijenga katika Kata ya Tinde, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, kwa lengo la kuwawezesha waendesha bodaboda kufanya shughuli zao katika mazingira salama na yenye utaratibu. Mbunge wa Jimbo la Itwangi, Mhe. Azza Hillal Hamad, akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa vituo vya waendesha bodaboda alivyovijenga katika Kata ya Tinde, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuwawezesha vijana kufanya shughuli zao k…