AJIRA ZA WAZAWA ZILINDWE : CI NYAKUNGA

AJIRA ZA WAZAWA ZILINDWE : CI NYAKUNGA
Na. OWM (KAM), Dar es Salaam Kamishna wa Uhamiaji wa Divisheni ya Usimamizi na Udhibiti wa Mipaka, CI Fakih Nyakunga, ameiomba Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano) kupitia Idara ya Kazi kuhakikisha vibali vya kazi vinatolewa kwa raia wa kigeni wenye ujuzi ambao haupatikani nchini Tanzania ili kulinda ajira za wazawa. Nyakunga ametoa kauli hiyo leo Julai 12, 2026, alipotembelea Banda Jumuishi la Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na taasisi zake katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) 2026. Amesema utoaji wa vibali kwa wataalamu wa kigeni wenye ujuzi adimu utatoa fursa kwa Watanzania kujifunza teknolojia na maarifa mapya kupitia ushirikiano kazini, jambo litakalosaidia kuongeza uwezo wa rasilimali watu na kuchochea maendeleo ya uchumi wa nchi. Aidha, Kamishna Nyakunga ameipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu kwa juhudi zake za kutafuta fursa za ajira kwa Watanzania nje ya nchi. Ameiomba Ofisi hiyo, kupitia Idara ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi, Sehemu ya Huduma za …