Airtel Tanzania Yawajengea Vijana Ujuzi wa Kubadili Taka za Kielektroniki kuwa Fursa za Biashara

Airtel Tanzania Yawajengea Vijana Ujuzi wa Kubadili Taka za Kielektroniki kuwa Fursa za Biashara
Airtel Tanzania inaendelea kutekeleza dhamira yake ya kuwawezesha vijana kupitia ujuzi wa kidijitali unaozingatia utunzaji wa mazingira. Hii imefanyika kupitia mafunzo ya urejeshaji na ukarabati wa vifaa vya kielektroniki yaliyotolewa wakati wa warsha ya ReFab Dar 2, iliyofanyika jijini Dar es Salaam kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Vijana na Stadi 2026. Warsha hiyo iliandaliwa kwa ushirikiano kati ya Dar Teknohama Business Incubator, BUNI Hub, Airtel Fursa Lab na TechStar Innovation Hub. Lengo lilikuwa kuwakutanisha wanafunzi wa vyuo vikuu, vyuo vya ufundi stadi, wahitimu wa TEHAMA, wajasiriamali na wabunifu ili kupata mafunzo ya vitendo kuhusu ukarabati wa vifaa, usimamizi wa taka za kielektroniki na mbinu salama za urejelezaji. Katika hatua ya kuimarisha mafunzo hayo, Airtel Tanzania imekabidhi jumla ya kompyuta 35 kwa DTBi. Pia kupitia ushirikiano wa Airtel Fursa Lab na DTBi, zaidi ya vijana na wajasiriamali 5,300 wamenufaika na mafunzo ya ujuzi wa kidijitali, ujasiriamali na uchumi…