AFRIKA KUUNGANA KUCHOCHEA MAENDELEO YA VIWANDA.

AFRIKA KUUNGANA KUCHOCHEA MAENDELEO YA VIWANDA.
Na. Saidina Msangi, WF, Abidjan, Côte d’Ivoire. Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mshamu Ali Munde (Mb), kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Pamoja wa 9 wa Kamati Maalum ya Mawaziri (STC) ya Umoja wa Afrika inayoshughulikia Fedha, Uchumi, Mipango na Mtangamano, pamoja na Mkutano wa 5 wa Kamati ya Mawaziri wa Biashara, Utalii, Viwanda na Madini. Mkutano huo wa kimkakati ulioanza rasmi tarehe 24 Julai 2026 jijini Abidjan, Côte d’Ivoire, unalenga kuweka misingi imara ya ushirikiano wa kiuchumi barani Afrika. Mkutano huo umejadili kwa kina umuhimu wa nchi za Afrika kuharakisha juhudi za kuendeleza sekta ya viwanda kwa kuongeza thamani ya malighafi za ndani badala ya kusafirishwa zikiwa ghafi, kuimarisha minyororo ya thamani ya kikanda, pamoja na kuweka mazingira bora na wezeshi yatakayovutia uwekezaji wenye tija kiuchumi. Wajumbe wa mkutano huo walibainisha kuwa, kutokana na Bara la Afrika kuwa na rasilimali nyingi za asil…