ZAIDI YA WANUFAIKA 17,000 WA KAYA MASKINI RUVUMA WAFIKIWA NA BIMA YA AFYA KWA WOTE.
ZAIDI YA WANUFAIKA 17,000 WA KAYA MASKINI RUVUMA WAFIKIWA NA BIMA YA AFYA KWA WOTE.
Meneja wa mfuko wa bima ya Afya Mkoa wa Ruvuma Hansi John Akizungumza na waandishi wa habari waliomtembelea ofisini kwake kuhusu mipango ya serikali kuzifikia kaya zisizo na uwezo na utekelezaji wake kwa awamu kupitia mpango wa TASAF. Na Regina Ndumbaro Songea-Ruvuma Mfuko wa Bima ya Afya Mkoa wa Ruvuma umefanikiwa kuwafikia zaidi ya wanufaika 17,000 kutoka kaya zisizo na uwezo katika utekelezaji wa awamu ya kwanza ya mpango wa Bima ya Afya kwa Wote unaotekelezwa na Serikali kupitia mpango wa TASAF. Meneja wa Mfuko wa Bima ya Afya Mkoa wa Ruvuma, Hansi John, amesema Serikali ilitoa nafasi ya kusajili zaidi ya kaya 11,000 mkoani humo na hadi sasa asilimia 53 ya kaya hizo zimefikiwa huku zoezi likiendelea katika wilaya zote za mkoa huo. Akizungumza ofisini kwake, Hansi amesema changamoto ya wakazi wengi wa Ruvuma kuwa mashambani katika shughuli za kilimo ilisababisha baadhi ya walengwa kushindwa kufikiwa kwa wakati, lakini sasa wananchi wengi wameanza kurejea vijijini jambo litakalowezes…