WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA YAHIMIZA VIJANA KUTUMIA FURSA ZA KIUCHUMI
WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA YAHIMIZA VIJANA KUTUMIA FURSA ZA KIUCHUMI Na. Meleka Kulwa-Fullshangwe Blog,Dodoma DODOMA: Wizara ya Viwanda na Biashara imewahimiza wananchi, hususan vijana na wajasiriamali, kutumia kikamilifu fursa zinazotolewa na taasisi zake ili kukuza biashara, kuongeza kipato na kuchangia maendeleo ya uchumi wa taifa. Wito huo umetolewa leo Juni 17, 2026 na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Saidi Msabimana, wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Chinangali jijini Dodoma. Msabimana amesema wizara hiyo, ambayo ni miongoni mwa taasisi muhimu katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, imeshiriki maonesho hayo pamoja na taasisi nane zilizo chini yake kwa lengo la kusogeza huduma karibu na wananchi pamoja na kutoa elimu kuhusu biashara, viwanda na uwekezaji. Amesema jukwaa hilo limetumika kuwafikia wananchi moja kwa moja kwa kuwapa taarifa za huduma zinazotolewa na kuwaelekeza namna ya kutumia fursa zilizopo kwa maendeleo yao binafsi na taifa kwa ujumla. “Tunatumia jukwaa h…