WAZIRI WA UTAMADUNI WA UAE ATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA JIJINI PARIS, ASISITIZA KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIDIPLOMASIA NA KIUTAMADUNI
WAZIRI WA UTAMADUNI WA UAE ATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA JIJINI PARIS, ASISITIZA KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIDIPLOMASIA NA KIUTAMADUNI Paris, Ufaransa – Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Ufaransa, Mheshimiwa Saidi Othman Yakubu, leo amepokea ugeni wa Mheshimiwa Sheikh Salem bin Khaled Al Qassimi, Waziri wa Utamaduni wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Elimu, Utamaduni na Sayansi ya UAE, aliyefanya ziara maalum katika Ubalozi wa Tanzania jijini Paris. Katika mazungumzo yao, viongozi hao walijadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na UAE, hususan katika sekta za utamaduni, elimu, sayansi, urithi wa dunia, ubunifu na diplomasia ya kimataifa kupitia taasisi za kimataifa zikiwemo UNESCO. Mheshimiwa Balozi Yakubu alieleza kuwa Tanzania na UAE zinaendelea kufurahia mahusiano ya karibu na ya kirafiki yaliyojengwa juu ya msingi wa kuheshimiana, ushirikiano wa kiuchumi na maono ya pamoja ya maendeleo endelevu. Alisisitiza dhamira ya Tanzania ya kuendelea kuimarisha ushirikiano na UAE katika nyanja za utamaduni na ubadilishanaji wa uzoefu wa kitaalamu. Kwa upande wa…