WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA SLOVAKIA AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI

WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA SLOVAKIA AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI
Waziri wa Mambo ya Nje na Masuala ya Ulaya wa Jamhuri ya Slovakia, Mhe. Juraj Blanár, amewasili nchini kwa ziara ya kikazi kuanzia Juni 10 hadi 11, 2026, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na ushirikiano kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Slovakia. Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam Mhe. Juraj Blanár alilakiwa na Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. James Milya (Mb). Akiwa nchini, Mhe. Blanár atashiriki katika mazungumzo ya pande mbili na mwenyeji wake, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) yatakayofanyika Juni 11 2026. Ziara hii inalenga kuimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali ikiwemo utalii, elimu, programu za ufadhili wa masomo, usalama wa mtandao, biashara na uwekezaji. Baada ya mazungumzo na mwenyeji wake watazungumza na waandishi wa habari na ba…