WAZIRI SANGU: SERIKALI KUENDELEA KUKUZA USTAWI WA SEKTA YA KAZI NA USHIRIKIANO KIMATAIFA
WAZIRI SANGU: SERIKALI KUENDELEA KUKUZA USTAWI WA SEKTA YA KAZI NA USHIRIKIANO KIMATAIFA
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu akisalimiana na Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Umoja wa Mataifa Nchini Uswisi, Mhe. Dkt. Abdallah Possi alipotembelea ofisi za Ubalozi huo leo Juni 3, 2026. Na: OWM (KAM) – Geneva, Uswisi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Deus Sangu leo Juni 3, 2026 amefanya mazungumzo Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Ofisi za Umoja wa Mataifa Mhe. Dkt. Abdallah Possi na kueleza azma ya Serikali katika azma ya kukuza Ustawi wa Sekta ya Kazi na kuimarisha Ushirikiano wa Kimataifa. Amesema hayo Juni 3, 2026 alipotembelea Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Uswisi, akiwa katika ziara yake ya kikazi nchini humo inayolenga kushiriki Mkutano Mkuu wa 114 wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) unaofanyika Jijini Geneva, Uswisi. Katika mazungumzo yao na Balozi Possi wamejadili ushiriki wa Tanzania katika Mkutano huo na manufaa yake makubwa kwa Taifa ikiwemo fursa za kuendeleza ushirikia…