WAZIRI SANGU: SERIKALI INATHAMINI MCHANGO WA TAASISI ZA DINI KATIKA KUJENGA AMANI NA MAENDELEO YA TAIFA
WAZIRI SANGU: SERIKALI INATHAMINI MCHANGO WA TAASISI ZA DINI KATIKA KUJENGA AMANI NA MAENDELEO YA TAIFA
SERIKALI imeendelea kuthamini mchango mkubwa unaotolewa na taasisi za kidini nchini katika kuimarisha amani, mshikamano na maendeleo ya taifa. Amesema hayo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Deus Sangu leo Juni 19,2026 alipomwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, katika ibada maalum ya kuliombea Taifa la Tanzania katika kanisa la KKKT Dayosisi ya Mashariki ya Ziwa Victoria Jijini Mwanza. Akizungumza katika ibada hiyo, Waziri Sangu amesema Serikali inatambua mchango muhimu wa taasisi za kidini katika kujenga jamii yenye maadili mema, umoja na mshikamano, mambo ambayo ni msingi wa maendeleo endelevu ya nchi. Amesema kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na wadau wote ikiwemo makundi mbalimbali ya kijamii yenye nia njema ya kuijenga Tanzania yetu. “Tunatambua kuwa maendeleo ya kweli hayawezi kupatikana bila amani, utulivu, umoja na mshikamano wa wananchi wake” Katika hatua nyingine Waziri Sangu amewahasa viongoz…