WAZIRI SANGU: MAHUSIANO, AMANI NA UMOJA NI MSINGI WA MAENDELEO YA TAIFA
WAZIRI SANGU: MAHUSIANO, AMANI NA UMOJA NI MSINGI WA MAENDELEO YA TAIFA
W aziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu amesema kuwa uamuzi wa Serikali ya Awamu ya Sita wa kuanzisha Wizara maalum yenye dhamana ya kushughulikia masuala ya Mahusiano inaakisi maono ya Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuimarisha Umoja, Mshikamano na Amani nchini. “Dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha Tanzania inaendelea kuwa taifa lenye amani, mshikamano na maendeleo kupitia mazungumzo, maridhiano na ushirikiano wa wadau wote,” amesema. Mhe. Sangu amesema hayo Juni 28, 2026 katika Ibada maalumu ya kilele cha harambee iliyofanyika kwenye ushirika wa Amani wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kati, mjini Singida ambapo alieleza kuwa Serikali imeendelea kujenga mazingira ya mazungumzo na ushirikiano kati yake na taasisi za dini ili kuimarisha mshikamano wa kitaifa. Alisema Ofisi ya Waziri Mkuu kuratibu Mahusiano ni utekelezaji wa maelekezo …