WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA AKERWA NA UTOAJI HAFIFU WA HUDUMA KWA WANANCHI ATAKA WATUMISHI KUTENDA HAKI.
WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA AKERWA NA UTOAJI HAFIFU WA HUDUMA KWA WANANCHI ATAKA WATUMISHI KUTENDA HAKI. NA DENIS MLOWE, IRINGA WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwigulu Nchemba, amewataka watumishi wa umma kote nchini kutoa huduma kwa wananchi kwa weledi, uadilifu na unyenyekevu, akisisitiza kuwa nafasi walizonazo ni za utumishi na si za kujionyesha mamlaka. Akizungumza katika mkutano wa kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa Jimbo la Ismani mkoani Iringa, Dkt. Nchemba alisema serikali haitavumilia tabia ya baadhi ya watumishi wanaowazungusha wananchi kwa kuwapa usumbufu usio wa lazima wakati wa kutafuta huduma katika ofisi za umma. Alisema wananchi wanaostahili kupata haki au huduma wanapaswa kuhudumiwa kwa wakati bila kucheleweshwa kwa sababu mambo ya urasimu usio na tija yamepitwa na wakati na yanachelewesha maendeleo ya wananchi pamoja na taifa kwa ujumla. Waziri Mkuu alieleza kuwa watumishi wa umma wanapaswa kutambua kuwa mishahara yao inatokana na kodi zinazolipwa na wananchi, hivyo wanawajibika kuwahudumia kwa heshima na kujituma. Alisema wananchi wengi hujinyima mahi…