WAZIRI MKUU ASEMA TANZANIA IKO SALAMA DHIDI YA UGONJWA WA EBOLA

WAZIRI MKUU ASEMA TANZANIA IKO SALAMA DHIDI YA UGONJWA WA EBOLA
Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Tanzania bado ni salama dhidi ya ugonjwa wa Ebola huku Serikali ikiendelea kuimarisha mifumo ya tahadhari, ufuatiliaji na utoaji wa elimu kwa wananchi kuhusu magonjwa ya mlipuko. Ametoa kauli hiyo leo Alhamisi, Juni 4, 2026 Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la papo kwa papo la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Asha Salum Moto, ambaye alitaka kujua namna Serikali ilivyojipanga kukabiliana na ugonjwa wa Ebola unaoripotiwa katika baadhi ya nchi jirani. "Mpaka sasa tuko salama, nchi yetu iko salama. Ni jambo la kumshukuru Mungu. Hata hivyo, kwa kuwa Tanzania si kisiwa, tunaendelea kuchukua hatua zote za tahadhari ili kuhakikisha usalama wa wananchi wetu unaendelea kuwepo," amesema Dkt. Mwigulu. Amesema Serikali inaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu namna ya kujikinga na magonjwa ya mlipuko, kuimarisha ufuatiliaji mipakani pamoja na kuhimiza utoaji wa taarifa mapema pale dalili za magonjwa hayo zinapojitokeza. "Tu…