WAZIRI MCHENGERWA AZINDUA BODI YA WADHAMINI YA JKCI, KUIMARISHA UTAWALA NA UENDELEVU WA TAASISI

WAZIRI MCHENGERWA AZINDUA BODI YA WADHAMINI YA JKCI, KUIMARISHA UTAWALA NA UENDELEVU WA TAASISI
Na Atley Kuni, WAF – Dar es Salaam Serikali kupitia Waziri wake wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa imezindua rasmi Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), hatua inayolenga kuimarisha utawala bora, uwajibikaji na usimamizi wa kimkakati wa taasisi hiyo muhimu katika utoaji wa huduma za moyo nchini. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika Juni 12, 2026 jijini Dar es Salaam, Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Mchengerwa, amesema kuanzishwa kwa Bodi hiyo ni sehemu ya juhudi za Serikali za kuhakikisha JKCI inaendelea kukua na kutoa huduma za kibingwa na kibingwa bobezi kwa viwango vya kimataifa. Amesema Bodi ya Wadhamini itakuwa chombo muhimu cha ushauri na usimamizi kitakachosaidia taasisi kupanga na kutekeleza mikakati ya muda mrefu, sambamba na kusimamia matumizi bora ya rasilimali kwa manufaa ya wananchi.  Mhe. Mchengerwa amesema kuwa katika kipindi ambacho JKCI imeendelea kupanua huduma zake na kupokea wagonjwa kutoka ndani na nje ya Tanzania, kunahitajika mfumo imara wa …