WAZIRI MASAUNI ASITISHA SHUGHULI ZA KIWANDA CHA AFRICAN STEEL KWA UCHAFUZI WA MAZINGIRA

WAZIRI MASAUNI ASITISHA SHUGHULI ZA KIWANDA CHA AFRICAN STEEL KWA UCHAFUZI WA MAZINGIRA
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhandisi Hamad Masauni, amesitisha shughuli za Kiwanda cha African Steel Group Company Limited kilichopo Kijiji cha Mwavi, Kata ya Fukayosi, Wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani, kinachotumia chuma chakavu kuzalisha nondo kwa ukiukwaji wa Sheria na Kanuni za uhifadhi wa mazingira. Hatua hiyo imefikiwa wakati wa ziara ya Waziri Masauni ya kukagua utekelezaji wa Sheria za mazingira katika viwanda vitatu vilivyopo Wilaya ya Bagamoyo, ambapo amekipongeza kiwanda cha KAMAL Refinery Limited kinachojishughulisha na uchakataji wa mafuta machafu na Roster Vehicle Equipment Limited kinachojihusisha na utengenezaji na uunganishaji wa magari (truck assembly) kwa Usimamizi mzuri wa Sheria ya Mazingira Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Waziri Masauni amesema Kiwanda cha African Steel kimeendelea kuchafua mazingira licha ya kupewa maelekezo mara kadhaa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kufuatia ukaguzi uliofany…