WAZIRI KAPINGA KUONGOZA KILELE CHA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA TBS.
WAZIRI KAPINGA KUONGOZA KILELE CHA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA TBS.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt. Ashura Katunzi,akitoa taarifa kwa umma kuelekea kuhitimisha maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwake Juni 19,2026 jijini Dodoma. ... Shirika la Viwango Tanzania (TBS) linatarajia kuandika historia mpya Juni 19, 2026 kwa kuhitimisha maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwake, huku likitarajia kuzindua kitabu maalumu kitakachobeba historia, mafanikio na mchango wake katika maendeleo ya viwanda, biashara na ustawi wa Watanzania. Akizungumza jijini Dodoma kuhusu maandalizi ya kilele cha maadhimisho hayo, Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt. Ashura Katunzi, amesema hafla hiyo itafanyika katika ofisi za shirika hilo na inatarajiwa kuhudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka sekta za umma na binafsi. Dkt. Katunzi amesema mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Salvio Kapinga (Mb), ambaye ataungana na viongozi, wadau na wananchi kusherehekea mafanikio ya nusu karne ya taa…