WATAALAMU WATAKA MIFUMO IMARA YA KULINDA RASILIMALI ZA UMMA
WATAALAMU WATAKA MIFUMO IMARA YA KULINDA RASILIMALI ZA UMMA Na Happy Lazaro, Arusha Serikali imezitaka taasisi za umma kuimarisha mifumo ya uwajibikaji, uwazi na udhibiti wa ndani ili kukabiliana na vitendo vya udanganyifu vinavyoathiri matumizi sahihi ya rasilimali za taifa na utoaji wa huduma kwa wananchi. Akifungua Kongamano la Uhamasishaji wa Kupambana na Udanganyifu katika Sekta ya Umma (Public Sector Fraud Awareness Forum) jijini Arusha, Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Dkt. Rahma Salim Mahfoudh, amesema mapambano dhidi ya udanganyifu yanahitaji ushirikiano wa karibu kati ya taasisi za umma, sekta binafsi na wataalamu wa uchunguzi, huku akisisitiza matumizi ya teknolojia za kisasa na mifumo madhubuti ya udhibiti ili kulinda rasilimali za taifa. Rais wa ACFE Tanzania Chapter, Aly Mbaruku Juma, amesema taasisi hiyo imeendelea kufanya tafiti za kitaalamu kuhusu mwenendo wa udanganyifu katika sekta mbalimbali kwa lengo la kusaidia taasisi kubaini maeneo yenye vihatarishi na kuimarisha mifumo ya usimamizi na uadilifu. Kwa upande wao,…