WASHAURI WA WANAFUNZI WATAKIWA KUENDANA NA MABADILIKO YA KIDIJITALI
WASHAURI WA WANAFUNZI WATAKIWA KUENDANA NA MABADILIKO YA KIDIJITALI
Na Oscar Assenga,TANGA SERIKALI imekipongeza Chama cha Washauri wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Tanzania (TACOGA) kwa kuendelea kuandaa mafunzo yanayolenga kuimarisha uwezo wa kitaaluma na kiutendaji wa washauri wa wanafunzi, wanasihi na viongozi wa serikali za wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali nchini. Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo yaliyofanyika jijini Tanga,Mkurugezi wa Maendeleo ya Jinsia kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalumu Badru Abdnur alisema mafunzo hayo yamekuwa jukwaa muhimu la kuwajengea washiriki uwezo wa kukabiliana na changamoto zinazowakabili wanafunzi katika taasisi za elimu ya juu. Alisema katika kipindi cha mafunzo hayo, washiriki walipata nafasi ya kujifunza, kubadilishana uzoefu na kujadili changamoto mbalimbali wanazokutana nazo katika utekelezaji wa majukumu yao, pamoja na kupata mbinu mpya zitakazowawezesha kuboresha huduma wanazozitoa kwa wanafunzi. "Nawapongeza viongozi wa TACOGA kwa ubunifu na maono yao ya kuhakikisha m…