Wanufaika 588 wa ‘NBC Wajibika Scholarship’ Waanza Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA
Wanufaika 588 wa ‘NBC Wajibika Scholarship’ Waanza Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA
Jumla ya vijana 588 wanaonufaika na mpango wa ufadhili wa mafunzo ya ufundi stadi kwa vijana wa ‘NBC Wajibika Scholarship’ wameanza rasmi mafunzo yao katika vyuo vya VETA Kihonda mkoani Morogoro na VETA Mwanza, huku Benki ya NBC ikisisitiza dhamira yake ya kuendelea kuwekeza katika maendeleo ya rasilimali watu kama njia ya kuchochea ukuaji wa uchumi jumuishi nchini. Mpango huo unatekelezwa kwa ushirikiano kati ya Benki ya NBC na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), ukiwa na lengo la kuwawezesha vijana kupata ujuzi unaowawezesha kujiajiri, kuajiriwa na hata kuwa waajiri, sambamba na kuunga mkono jitihada za Serikali za kujenga uchumi shindani unaotegemea nguvu kazi yenye ujuzi, ubunifu na tija. Hafla ya uzinduzi wa utekelezaji wa mpango huo ilifanyika jana katika Chuo cha VETA Kihonda, ambapo wanafunzi 294 wanapatiwa mafunzo, huku idadi kama hiyo ikinufaika katika Chuo cha VETA Mwanza. Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa VETA wakiongozwa na Mkurugenzi wa VETA…