WANAFUNZI WA MRIJO JUU WANUFAIKA NA MSAADA WA VIFAA VYA HEDHI KUIMARISHA ELIMU YA WASICHANA
WANAFUNZI WA MRIJO JUU WANUFAIKA NA MSAADA WA VIFAA VYA HEDHI KUIMARISHA ELIMU YA WASICHANA
Na Janeth Raphael - MichuziTv Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Mrijo Juu iliyopo wilayani Chemba mkoani Dodoma wamepata nafuu ya changamoto zinazowakabili wakati wa hedhi baada ya kupatiwa msaada wa vifaa maalumu vinavyoweza kutumika kwa muda mrefu, hatua inayolenga kuwawezesha kuendelea na masomo bila kukatishwa tamaa au kukosa vipindi vya darasani. Msaada huo umetolewa na TotalEnergies Tanzania kwa kushirikiana na mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), ukiwa sehemu ya juhudi za kuimarisha elimu ya mtoto wa kike na kuhakikisha anabaki shuleni hadi kukamilisha masomo yake. Kila mwanafunzi alinufaika na kifurushi chenye taulo za kike zinazoweza kufuliwa na kutumika tena kwa muda wa zaidi ya miaka mitatu, pamoja na sabuni, nguo za ndani na ndoo kwa ajili ya kusaidia usafi na uhifadhi wa vifaa hivyo. Vifaa hivyo vinalenga kupunguza changamoto za upatikanaji wa pedi za mara kwa mara pamoja na kusaidia usafi wa mazingira. Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuruge…