WANAFUNZI ATC WAGUNDUA MASHINE KUPIGA KURA KIDIGITALI, WATAKIWA KUSOMA DIRA 2050
WANAFUNZI ATC WAGUNDUA MASHINE KUPIGA KURA KIDIGITALI, WATAKIWA KUSOMA DIRA 2050
Na Seif Mangwangi, Michuzi TV Arusha WANAFUNZI wanaofanya ubunifu wa matumizi ya teknolojia mbalimbali katika chuo cha ufundi Arusha (ATC), wametakiwa kusoma Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kuielewa na kuona fursa zilizopo ndani yake na kufanya bunifu zao kutokana na malengo ya dira hiyo. Hayo yameelezwa Juni 19, 2026 na Mkuu wa chuo cha ufundi Arusha Profesa Musa Chacha katika hotuba yake ya kufungua wiki ya maonyesho ya ubunifu yanayoandaliwa kila mwaka chuoni hapo. Profesa Chacha amesema dira ya Taifa 2050 imeainisha maeneo ambayo yanapaswa kuendelezwa kwaajili ya Maendeleo ya Watanzania hivyo wanafunzi wanaofanya bunifu chuoni hapo wanapaswa kuyasoma na kuyajua na kuyafanyia ubunifu. Amesema kutokana na kazi nzuri ya ubunifu ambayo imekuwa ikifanywa na wanafunzi chuoni hapo, chuo kimepanga kujenga jengo maalum la ghorofa nne ambalo litatumika kwaajili ya shughuli za ubunifu. “ Kwa kushirikiana na Serikali ya Italia hivi karibuni tunatarajia kujenga jengo kubwa la ghorofa nne ambalo l…