WALIPAKODI DODOMA WACHANGAMKIA HUDUMA ZA OFISI INAYOTEMBEA YA TRA.
WALIPAKODI DODOMA WACHANGAMKIA HUDUMA ZA OFISI INAYOTEMBEA YA TRA.
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Dodoma imeendelea kusogeza huduma zake karibu na wananchi kupitia Ofisi Inayotembea, hatua inayolenga kurahisisha upatikanaji wa huduma za kodi na kuwasaidia walipakodi kutimiza wajibu wao kwa ufanisi. Akizungumza wakati wa utoaji wa huduma hizo, Meneja wa TRA Mkoa wa Dodoma, Pendolake Elinisafi, amesema Ofisi Inayotembea ni sehemu ya mkakati wa TRA wa kuwafikia wananchi moja kwa moja katika maeneo yao ili kuwapatia huduma mbalimbali za kikodi bila kulazimika kufika katika ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania. Ameeleza kuwa huduma zinazotolewa kupitia Ofisi Inayotembea ni pamoja na usajili wa Namba za Utambulisho wa Mlipakodi (TIN), utoaji wa elimu ya kodi, ushauri wa masuala mbalimbali ya kikodi pamoja na utatuzi wa changamoto zinazowakabili walipakodi. Elinisafi amewahimiza wananchi na wafanyabiashara wa Mkoa wa Dodoma kutumia fursa hiyo kwa kujitokeza kwa wingi ili kupata huduma na maelezo sahihi yatakayowawezesha kutekeleza wajibu wao wa kulipa…