Walimu Bora wa Dodoma Waenda Korea Kusini Kusaka Maarifa Mapya.

Walimu Bora wa Dodoma Waenda Korea Kusini Kusaka Maarifa Mapya.
Na Mwandishi Wetu UJUMBE wa walimu na viongozi wa elimu kutoka Mkoa wa Dodoma wapatao 40 umeondoka kwenda Korea Kusini kujifunza mbinu za kisasa za ufundishaji, usimamizi wa shule na matumizi ya teknolojia katika elimu. Walimu hao wanatarajiwa kushiriki mafunzo na ziara ya kielimu ya siku nne ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wao katika kuongeza ufaulu wa wanafunzi mkoani humo. Mratibu wa safari hiyo na Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link, Abdulmalik Mollel, amesema walimu hao waliondoka kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kuelekea Seoul, Korea Kusini, kupitia Doha, Qatar. Amesema katika ziara hiyo washiriki watajifunza namna Korea Kusini inavyotumia teknolojia, ubunifu, nidhamu na usimamizi bora katika kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji. Pia watapata uzoefu kuhusu matumizi ya mifumo ya kidijitali darasani, maandalizi ya masomo na ufuatiliaji wa maendeleo ya wanafunzi. Amesema kabla ya kuondoka walipatiwa mafunzo ya maandalizi kuhusu utamaduni wa Korea Kusin…