WAKULIMA WA MIWA MVOMERO NA KILOSA WAPATIWA MAFUNZO MATUMIZI SALAMA YA VIUATILIFU
WAKULIMA WA MIWA MVOMERO NA KILOSA WAPATIWA MAFUNZO MATUMIZI SALAMA YA VIUATILIFU
Na Mwandishi Wetu. WAKULIMA wa zao la miwa katika wilaya za Mvomero na Kilosa mkoani Morogoro wamehimizwa kutumia viuatilifu kwa usahihi na kufuata taratibu za usalama ili kujikinga na madhara yanayoweza kuathiri afya zao pamoja na mazingira. Rai hiyo imetolewa na Mtafiti kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) Kituo cha Kibaha, Ngabo Vicent Pamba wakati wa mafunzo maalumu yaliyofanyika eneo la Mtibwa wilayani Mvomero, yakihusisha wakulima wa miwa, maafisa ugani, wauzaji wa pembejeo za kilimo pamoja na maafisa wa mazingira. Ngabo amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wadau mbalimbali wa mnyororo wa thamani wa zao la miwa kuhusu matumizi sahihi ya viuatilifu na namna salama ya kuhifadhi na kutupa vifungashio vya viuatilifu baada ya matumizi. “Tuko hapa kutoa mafunzo mahususi kwa wakulima, maafisa ugani, wauzaji wa pembejeo na maafisa wa mazingira kuhusu matumizi sahihi ya viuatilifu pamoja na uhifadhi salama wa vifungashio vyake. Lengo ni kuiepusha jamii ya wakulim…