WAHITIMU TPSC WAHIMIZWA KUCHANGIA UTEKELEZAJI DIRA 2050
WAHITIMU TPSC WAHIMIZWA KUCHANGIA UTEKELEZAJI DIRA 2050
Na. Jawadu Kinyobwa – Mtwara Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete (Mb), amewataka wahitimu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kutumia maarifa, ujuzi na stadi walizopata chuoni kuchangia maendeleo ya Taifa na kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. Akizungumza wakati wa Mahafali ya 43 ya Chuo TPSC Kampasi ya Mtwara, yaliyofanyika leo Juni 13, 2026, Mhe. Kikwete amewapongeza wahitimu 1,926 waliohitimu katika ngazi ya Astashahada, Stashahada na Shahada ya Kwanza kwa juhudi, nidhamu na uvumilivu uliowawezesha kufikia mafanikio hayo. Alisema kuwa kuhitimu masomo si mwisho wa kujifunza bali ni mwanzo wa safari mpya ya kuitumikia jamii na Taifa, huku akiwataka wahitimu kuwa mabalozi wazuri wa Chuo kwa kuzingatia maadili, uwajibikaji, uzalendo na ubunifu katika maeneo yao ya kazi na maisha ya kila siku. “Taifa linahitaji wataalamu wenye uwezo wa kutatua changamoto, kuleta ubunif…