WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUTOA ELIMU YA USALAMA WA MTOTO MTANDAONI
WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUTOA ELIMU YA USALAMA WA MTOTO MTANDAONI Na John Bukuku, Dar es Salaam. Waandishi wa habari na waandaaji wa vipindi vya watoto nchini wametakiwa kutumia vyombo vyao vya habari kuelimisha jamii kuhusu usalama wa watoto mtandaoni ili kukabiliana na ongezeko la vitendo vya ukatili na matumizi mabaya ya teknolojia yanayowaathiri watoto. Wito huo umetolewa na Afisa wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari Tanzania, Prudence Constantine, alipokuwa akifungua mafunzo ya siku mbili kwa waandishi wa habari na waandaaji wa vipindi vya watoto kuhusu ulinzi na usalama wa mtoto mtandaoni yaliyofanyika jijini Dar es Salaam. Prudence alisema maendeleo ya teknolojia ya habari na mawasiliano yameleta manufaa makubwa katika upatikanaji wa taarifa, elimu, burudani na biashara, lakini pia yameongeza hatari mbalimbali zinazowakabili watoto wanapotumia mitandao bila uangalizi wa kutosha. Alisema waandishi wa habari wana jukumu muhimu la kuelimisha wazazi, walezi na jamii kuhusu matumizi salama ya mtandao pamoja na madhara yanayoweza kuwapata watoto…