WAAJIRI WANAOZINGATIA SHERIA ZA KAZI WAPONGEZWA

WAAJIRI WANAOZINGATIA SHERIA ZA KAZI WAPONGEZWA
Na OWM-KAM, Mwanza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano), Mhe. Deus Sangu, amepongeza waajiri nchini wanaotekeleza wajibu wao kwa kuzingatia sheria za kazi, ikiwemo kuwasilisha michango ya wafanyakazi katika Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kwa lengo la kulinda maslahi ya wafanyakazi dhidi ya madhara yanayotokana na kazi. Mhe. Sangu ametoa pongezi hizo leo Juni 18, 2026, jijini Mwanza wakati wa ziara yake ya kikazi katika viwanda vya Ziwa Steel na Nyanza Bottling Company, ambapo alijionea utekelezaji wa sheria za kazi na ustawi wa wafanyakazi katika maeneo hayo ya uzalishaji. Amesema kampuni hizo ni mfano mzuri wa kuigwa kutokana na namna wanavyotekeleza wajibu wa kuwasajili wafanyakazi katika mifuko ya hifadhi ya jamii na kuwasilisha michango yao kwa wakati, hatua inayochangia kulinda maslahi ya wafanyakazi na kuimarisha mahusiano bora kazini. “Serikali imeendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa sheria za kazi ili kuhakikisha wafanyakazi wanapata haki za…