VYOMBO VYA HABARI VYA MTANDAONI ‘KINARA’ KUWASILISHA KAZI ZA KUWANIA TUZO ZA SAMIA KALAMU 2026

VYOMBO VYA HABARI VYA MTANDAONI ‘KINARA’ KUWASILISHA KAZI ZA KUWANIA TUZO ZA SAMIA KALAMU 2026
Dar es Salaam, Juni 17, 2026 – Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kwa kushirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) na Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), imewahimiza waandishi wa habari na vyombo vya habari nchini kuendelea kuwasilisha kazi zao za kuwania Tuzo za Samia Kalamu 2026 kabla ya kufungwa kwa dirisha la maombi mwishoni mwa mwezi huu. Taarifa iliyotolewa jijini Dar es Salaam imeeleza kuwa hadi Juni 15, 2026, jumla ya kazi 624 zilikuwa zimewasilishwa kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini, huku vyombo vya habari mtandaoni vikiongoza kwa idadi kubwa ya kazi zilizowasilishwa. Takwimu zinaonyesha kuwa vyombo vya habari mtandaoni vimewasilisha kazi 276, sawa na asilimia 44 ya kazi zote zilizopokelewa. Magazeti yamewasilisha kazi 178 (asilimia 29), televisheni kazi 102 (asilimia 16), redio kazi 60 (asilimia 10), huku majarida yakichangia kazi nane pekee, sawa na asilimia moja ya jumla ya mawasilisho. Waandaaji wa tuzo hizo wameeleza kuwa …