VYOMBO VYA HABARI VILINDE MASLAHI YA WATOTO KATIKA UTOAJI WA TAARIFA

VYOMBO VYA HABARI VILINDE MASLAHI YA WATOTO KATIKA UTOAJI WA TAARIFA
Na John Bukuku, Dar es Salaam   Waandishi, watangazaji na waandaji wa vipindi vya watoto wametakiwa kuzingatia maadili na kanuni za kitaaluma katika kuripoti masuala ya watoto ili kulinda usalama, haki na ustawi wao. Akizungumza wakati wa kuwasilisha mada katika mafunzo ya siku mbili kwa waandaji na watangazaji wa vipindi vya watoto kuhusu malezi yaliyofanyika katika Ukumbi wa Afed jijini Dar es Salaam na kuhitimishwa leo Juni 18, 2026, Mtaalamu wa Mawasiliano na Utetezi wa UNICEF Tanzania, Usia Nkhoma Ledama, alisema vyombo vya habari vina jukumu kubwa zaidi ya kutoa taarifa kwani vinapaswa pia kutetea maslahi ya watoto na kuhakikisha sauti zao zinasikika kwa manufaa ya maendeleo yao. “Jukumu la vyombo vya habari katika kuripoti masuala ya watoto si kutoa taarifa pekee, bali pia kutetea maslahi yao, kuimarisha sauti zao na kuhakikisha kuwa simulizi zao zinaleta mabadiliko yenye manufaa katika jamii,” alisema Ledama. Alisisitiza kuwa kuripoti habari zinazowahusu watoto na vijana hakupaswi…